The House of Favourite Newspapers

BABA DIAMOND ADAIWA KUTELEKEZA MTOTO!

MAKUBWA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa kudaiwa kumtelekeza mtoto wake wa kiume aliyejitambulisha kwa jina la Emmanuel.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Godfrey, mkazi wa Magomeni, alisema Ijumaa iliyopita alimpokea Emmanuel akilalamika kuwa ana njaa akamnunulia chakula akala, lakini alipomaliza tu akaomba amkutanishe na baba Diamond kwani ndiye aliyekuwa akimtafuta.

“Ilikuwa siku ya Ijumaa saa moja usiku alikuja kijana mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la Emmanuel lakini nilipomuangalia alikuwa anaonekana kama ni mtu aliyechoka sana, alafu ana njaa kwa hiyo nilichokifanya nilienda kumnunulia chakula.

“Alipomaliza kula akaniomba nimkutanishe na baba Diamond kwa madai kwamba mama yake alimwambia kuwa huyo ndiye baba yake mzazi kwani alimtelekeza tangu akiwa mdogo kwa hiyo ametoka Kigoma na kuja Dar kumtafuta,” alisema Godfrey.

Ili kuujua ukweli wa habari hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta baba Diamond ambapo alikiri kumpokea kijana huyo na kusema kwamba siyo mtoto wake kama mwenyewe anavyodai bali ni kijana tu ambaye alikuwa anatafuta njia ya kukutana na Diamond kwa hiyo akaona njia rahisi ya kumfikia ni kujifanya mtoto wake.

 

“Nilikuwa katika pilikapilika zangu, mara nikapigiwa simu nikaambiwa kuwa kuna mgeni wangu nyumbani, nilipouliza ni nani nikaambiwa ni ndugu yake Diamond ambaye ni muimbaji pia katokea Kigoma.

“Baada ya kumaliza pilika zangu nilirudi nyumbani na kweli nikamkuta kijana huyo lakini cha kushangaza alikuwa anatetereka sana kujibu maswali kwa sababu hata nilipomuuliza jina la baba yake alitaja lingine kabisa tofauti na langu.

“Na kwa kuwa ilikuwa usiku nikaona si vema nikamruhusu aondoke hivyo nikamchukua mpaka nyumbani kwa mjumbe, lakini tulipofika pale mjumbe alikataa kuamka, basi tulirudi nyumbani nikamwambia alale hapo kutakapopambazuka ndiyo aondoke.

“Kabla asubuhi haijafika, nilikuja kugongewa mida ya saa sita usiku na mjumbe kuwa uyo kijana karuka geti na anataka kuiba vioo vya magari ya watu yaliyokuwa yamepaki nje, walitaka wampige lakini niliwaomba wasifanye hivyo, wakamuachia akaondoka na mpaka sasa sijui alipo.

“Unajua huyu siyo kijana wa kwanza kuja na kudai kuwa mimi ni baba yao, wanatafutaga njia ya kutaka kuonana na Diamond lakini wanashindwa kutokana na mama yake kule ni mkali hawawezi kuingia, kwa hiyo wanataka waje kwangu kwa sababu wanajua nafika kwa Diamond.

“Wanahisi wakidanganya hivyo itakuwa rahisi mimi kuwakutanisha kitu ambacho hakiwezekani, narudia tena mimi sina mtoto wa nje kwa sababu watoto wangu wote nawafahamu,” alisema baba Diamond.

STORI: Memorise Richard, DAR

Comments are closed.