The House of Favourite Newspapers

Baba Diamond Ammwagia Sifa Mme wa Mwenzake

0

 

DAR: Kiroho safi! Hicho ndicho kinachotokea kufuatia baba mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Jumaa ‘Baba D’ kuibuka na kummwagia sifa mume mwenzake; Maisara Abdul ‘Shamte’.

 

Shamte ndiye mume wa sasa wa mama Diamond au Mondi, Sanura Kassim ‘Sandra’.

Baba D ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, anamkubali kinoma Shamte kwani anaisimamia vizuri familia ya Mondi na hana kinyongo naye kwa sababu kila mmoja anapewa haki yake.

 

“Ninampongeza sana Shamte kwa sababu anaisimamia familia vizuri, sina kinyongo naye kwa sababu kila mtu ana maisha yake.

“Acheni wale maisha maana ni wakati wao! Maadam napata haki yangu kama baba, sioni ubaya kumsifia,” amesema.

 

Hivi karibuni picha za Baba D na Shamte zilizua gumzo la aina yake mitandaoni, kwani walionekana wakiwa pamoja huku wakicheka, yaani wakionekana wenye furaha ya aina yake kwenye sherehe ya mwanamuziki, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ ambaye ni dada wa Mondi.

 

Watu mbalimbali walionekana kushangazwa na ukaribu wa Baba D na Shamte huku wengine wakisema, Baba D anatakiwa kupewa tuzo kwani anachokifanya hakuna mwanaume anayeweza kuwa na moyo wa aina hiyo.

 

“Dah, huyu Baba D ana moyo wa kipekee sana maana anavyopendana na mume mwenzake Shamte hakuna mfano. Yaani wanakutana sherehe za watoto wake halafu wanashirikiana kwa kila kitu. Kiukweli Baba D anastahili tuzo,” aliandika mmoja wa mashabiki kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

 

Baba D na Shamte, mara ya kwanza walikutana kwenye 40 ya mtoto wa Diamond na Tanasha Donna na kushirikiana.

Mara ya pili ni kwa Queen Darleen hivi karibuni alipofanya sherehe ya ndoa yake baada ya kuolewa na mfanyabiashara Isihaka Mtoro.

Stori: Gladness Mallya,

Leave A Reply