BABA DIAMOND AMSAMEHE QUEEN DARLEEN

Abdul Juma

BABA mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amedaiwa kulainishwa na zawadi za Sikukuu ya Idd na kumsamehe binti yake, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’ ambaye walikuwa hawaivi.

 

Juni 8, mwaka huu, Queen alitupia posti kwenye akaunti yake ya Instagram iliyoashiria kuwathamini wazazi kwa kuwanunulia zawadi za sikukuu ya Idd, huku akionesha hofu kwa yeye kupokelewa zawadi zake na mzee Abdul kutokana na ugomvi waliokuwa nao.

 

“Allah sijui kama mzee Abdul atakubali zawadi zangu, Ramadhan kareem,” ilisomeka posti hiyo. Mtoa ubuyu mmoja ambaye yupo jirani na mzee Abdul alieleza kuwa, mara baada ya mzee huyo kuoneshwa posti hiyo aliamua kumsamehe fasta.

Ijumaa Wikienda lilimtafuta mzee Abdul na kumuuliza kama kweli amemsamehe bintiye huyo, akafunguka: “Yule mimi ni binti yangu, japo hapo awali tulikorofishana mpaka vyombo vya habari vikajua, lakini kama ataamua kuja kuomba msamaha nitampokea na mtoto akishaomba msamaha huwezi ukamkatalia kama kweli ataniletea zawadi nitazipokea na nitazitumia,” alisema mzee Abdul.

 

Queen aliingia kwenye bifu kali na mzee Abdul baada ya mrembo huyo kuhojiwa na televisheni moja ya mtandaoni kisha kusema, anamtambua Diamond kama baba yake mzazi na si mzee Abdul. Baba Diamond aliposikia hayo, alimtaka mrembo huyo asisogelee kaburi lake endapo atatangulia yeye mbele za haki.

MEMORISE RICHARD.

MPAKA HOME: MAISHA HALISI YA MWARABU FIGHTER, BAUNSA WA DIAMOND

Toa comment