The House of Favourite Newspapers

Baba Diamond kutua Sauzi

baba-diamond-1DA ES SALAAM: Baada ya juzikati kupatikana taarifa kuwa mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amepatana na baba yake mzazi, Abdul Juma, inadaiwa kuwa katika sherehe ya kutimiza siku 40 ya mtoto wa Diamond aitwaye Nillan ‘Chibu Junior’, babu mtu huyo naye atatinga Sauzi.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa Diamond aliyeomba hifadhi ya jina lake, baba Diamond ni kati ya watu watakaopata nafasi ya kukwea pipa kwenda Sauzi kwenye tukio hilo linalotarajiwa kuchukua nafasi Januari 16, mwaka huu.

diamond-na-zari“Sherehe ya kumtoa Nillan inatarajiwa kufanya Johannesburg, kule kwenye mjengo wa Diamond. Watu kadhaa kutoka Bongo wakiwemo mastaa wamepewa mualiko na utakuwepo usafiri maalum wa ndege wa kwenda na kurudi Sauzi.

“Nilimsikia Diamond akisema hata mzee Abdul atapata fursa ya kwenda kuwaona wajukuu zake, kwa hiyo tusubiri tuone,” alisema mtoa habari huyo.

Katika kuweka uzani wa habari hii, mwandishi wetu alifanya jitihada za kumpata Diamond lakini simu yake haikuweza kupatikana mara moja.

Ijumaa lilipata fursa ya kuzungumza na baba Diamond na kuulizwa kama ana taarifa juu ya safari hiyo ambapo alisema: “Hata mimi nasikiasikia ila kama itakuwa hivyo litakuwa ni jambo zuri kwani nitapata nafasi ya kuwaona wajukuu zangu. Kama nilivyosema, mimi na Diamond hakuna shida tena kwa hiyo hata hilo la kwenda Sauzi linawezekana kabisa.”

Comments are closed.