Baba Diamond: Queen Darleen naye kanisusa

Baba mzazi wa Diamond Platnumz, Abdul Juma.

MAYASA MARIWATA NA GLADNES MALLYA

BABA wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Juma amesema kuwa, anaumia kuona hata binti yake Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’ sasa kamsusa kama ilivyo kwa kaka yake (Diamond).

Queen Darleen.

Akizungumza na paparazi wetu, Mzee Abdul alisema: “Nashindwa kuelewa nini kimemsibu binti yangu huyu maana kipindi cha nyuma alikuwa anakuja kuniona mara kwa mara, lakini tangu aanze kuwa karibu na Diamond ambaye hanaga ‘taimu’ na mimi japo ni baba yake, kakata mawasiliano na mimi, hanijali kwa chochote hata nikimpigia simu hapokei.”

Baada ya kunasa malalamiko hayo, Queen Darleen alitafutwa na alipopatikana alisema: “Hahaa baba bwana! Nilijua lazima atalalamika, mimi nipo naye sambamba mwanzo mwisho, hakuna tatizo lolote na asihofu ila mara nyingi akinipigia nakuwa bize.”

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Toa comment