BABA KANUMBA TUMUOMBEE, AFANYIWA OPARESHENI!

TUMUOMBEE! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na baba wa aliyekuwa staa wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba anayeishi mkoani Shinyanga kuwa hoi kitandani kwa maradhi yaliyosababisha kufanyiwa oparesheni.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu hivi karibuni, baba Kanumba alieleza kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo na kibofu cha mkojo na kwamba amefanyiwa upasuaji ambapo anaendelea na matibabu mpaka sasa.

 

Aliendelea kusema kuwa kutokana na maradhi hayo kwa sasa anakula vyakula vya kuchagua kwani vingi madaktari wamemkataza asivitumie kwa kuwa vinaendelea kumuumiza. “Kwa sasa ninaendelea vizuri, nina nafuu kikubwa ni kuniombea tu ili nirudi kama kawaida, nilifanyiwa oparesheni ya tumbo mwezi mmoja uliopita na ninaendelea na matibabu.

“Kuna vyakula nimeambiwa nisile kwa sababu vitaniumiza zaidi kwa kuwa nina vidonda vya tumbo na mpaka nilipozidiwa nilikula vyakula ambavyo sitakiwi kula. “Pia nimegundulika kuwa nina tatizo kwenye kibofu cha mkojo, ndivyo walivyosema madaktari,” alisema baba Kanumba


Loading...

Toa comment