Baba Levo Akiri: Teacher ya Harmonize Ndio Amapiano Bora

NI headlines za mtangazaji kutoka kwa mwanamuziki Baba Levo, ambae amekiri kuwa katika mwaka 2021 katika nyimbo za #Amapiano wimbo wa #Teacher’ ulioimbwa na Harmonize ulikua wimbo mkali zaidi wa #Amapiano nchini Tanzania.
B’levo a.k.a. Fundi Majumba amethibitisha hilo kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, huku akimpinga mwanamuziki Marioo kuwa kama kungekuwa na tuzo basi singepata tuzo hata moja, kwa madai ya kuwepo kwa ngoma kali za #Amapiano kumzidi yeye.
Baba Levo ameushangaza umma wa mashabiki wa muziki Bongo kwani amekuwa mstari wa mbele kuuponda muziki wa Harmonize akusifia muziki wa Diamond lakini leo imekuwa tofauti kidogo kumsifia hasimu wake.
Unakubaliana na mtazamo wake..?!

