Baba Levo: Rayvanny Hajalipa Pesa Za WCB, Namshauri Alipe Aende Zake

Rayvanny

MSANII maarufu wa Bongo Fleva ambaye pia ni Official Chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo amesema kuwa licha ya kujiondoa ndani ya lebo ya WCB, msanii Rayvanny bado hajailipa lebo hiyo pesa zake kwa mujibu wa mkataba ili awe huru kufanya kazi zake.

 

Baba Levo amesema kuwa kazi zote za muziki za Rayvanny bado ziko chini ya WCB mpaka atakapolipa pesa hizo na kwamba hana namna nyingine ya kufanya zaidi ya kulipa pesa za watu.

 

“Diamond na Rayvanny kupelekana BASATA ni mambo ya kawaida katika kutafuta haki. Lakini nikuibieni tu ni kwamba, Rayvanny bado hajalipa hela anayodaiwa WCB, kwa hiyo ni hekaheka.

Baba Levo

“Rayvanny nii rafiki yangu lakini bado kuna vitu havijakaa sawa, tuwaache wakae na management watajua namna ya kumalizana, sababu wakati wanasaini mikataba hatukuwepo.

 

“Rayvanny ameshapewa go ahead na Diamond alipe pesa ili aondoke zake, lakini hajalipa. Mpaka sas, Rayvanny vitu vyake vinasimamiwa na WCB, sababu bado hajalipa hela, akilipa hela ataenda zake. Sasa hujalipa hela utakuwa independent vipi? Namshauri awape hela zao aendelee na mambo yake,” amesema Baba Levo.

4231
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment