The House of Favourite Newspapers

BABA: MONDI ATAPATA TAABU SANA!

LICHA ya hivi karibuni staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kumposti baba yake, Abdul Jumaa kwa mara ya kwanza kwenye ukurasa wake wa Instagram, mzee huyo ameibuka na kusema akifa mwanaye huyo atapata tabu sana.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, baba Diamond alisema aliiona picha hiyo ambayo mwanaye huyo aliiweka ambayo waliipiga wakiwa pamoja yaani yeye, mama Diamond na Diamond mwenyewe kipindi hicho akiwa mtoto.

 

Aliendelea kusema kwamba, kutokana na Diamond kushindwa kumsaidia inavyostahili na kutomjali kipindi hiki akiwa hai, siku akifariki dunia atapata tabu sana kwani atatamani angekuwepo lakini haitawezekana tena.

“Niliiona hiyo picha na nilijisikia kawaida na niliiona ni nzuri, haina tatizo lolote pia Diamond mimi ni baba yake hata iweje na ninajua ananichukia sasa hivi kwa kuwa bado ananiona niko hai lakini atakuja kupata taabu sana pindi nitakapokufa,’’ alisema baba Diamond.

 

IKO HIVI

Wiki iliyopita Diamond aliweka picha ya zamani akiwa mdogo inayomuonyesha akiwa na mama yake Sanura Kassim ‘Sandra’ na baba yake, Abdul wakiwa wametokelezea ile mbaya ambapo wafuasi wake wengi walionekana kumpongeza huku wengine wakimshushua kuwa inakuwaje sasa anamposti wakati alishasema kwamba baba huyo alimtelekeza.

“Huyu baba walimsingizia kuwa kamtelekeza Diamond mbona hapo wapo wote na anaonekana alikuwa mkubwa tu, huyu Bi Sandra kuna chuki aliipandikiza kati ya mtoto na baba, si mnaona anavyotaka kuipandikiza pia kwa deeylan (mtoto wa Mobeto) na baba ake,’’ aliandika mmoja wa mashabiki kwenye posti hiyo.

 

Mara kadhaa baba Diamond amenukuliwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari akimlalamikia mwanaye kwamba hamsaidii inavyostahili huku akitolea mfano kipindi hiki ambacho anasumbuliwa na tatizo la miguu achilia mbali kutokuwa na uhakika wa kula msosi wa maana.

STORI: Memorise Richard, DAR  

Comments are closed.