The House of Favourite Newspapers

Baba P… Baba Pili… Baba Pilima! “

Samahani kaka, sijui hiki kiti kina mtu?” aliuliza Kate au maarufu kwa jina la mama Pilima!

Ilikuwa kwenye baa ya Dolphin, iliyopo kwenye Jiji la Tanga maeneo ya Kwaminchi…

“Hapana anti, unaweza kuchukua tu maana aliyekaa ameshaondoka,” alijibu mwanaume mmoja aliyekutwa amekaa kwenye kiti pembeni ya meza hiyo.

Mama Pilima alikichukua kiti hicho na kuanza kutafuta meza nyingine tupu ili akae lakini akaikosa, akarudi na kiti mpaka kwenye meza hiyo kwa sababu mwanaume huyo alikaa peke yake…

“Samahani tena! Naweza kukaa hapa!”

“Unaweza kukaa tu maana hakuna mtu mwingine atakayekuja kukaa.”

Mama Pilima aliweka kiti hapo na kukaa kisha akaangalia upande walipokaa wahudumu lakini kwa bahati, mhudumu mmoja alisimama nyuma yake akisubiri akae ili amsikilize…

“Anti naomba bia ya baridi sana.”

“Bia gani?”

“Ooo! Lete Mount Meru.”

Wakati mhudumu ameondoka, mama Pilima alimgeukia yule mwanamke huku akijipepea kwa kitambaa kupunguza jasho…

“Samahani kwa usumbufu lakini,” alisema mama Pilima.

“Wala usijali,” alisema yule mwanaume huku akimwangalia mama Pilima kwa macho ya kumtathmini. Kila jicho lake lilipotua, ilikuwa moyoni akis    ema, ‘lakini umeumbwa! Utakuwa umeolewa kweli wewe? Mbona kama nimevutika na wewe!’

Na mama Pilima naye alipokutana macho na mwanaume huyo alimwangalia kama anayesema, ‘ukinitongoza nitakubali, lakini siwezi kukuanza maana naona unanitamani sana.’

Wakati wawili hao kila mmoja akimuwaza mwenzake kufuatia kumtamani kimahaba bia ililetwa.

Mama Pilima aliimimina yote kwenye glasi kubwa maana alikuwa na kiu sana. Aliipiga yote kwa mpigo huku macho yakiwa kwa mhudumu kama anayesema, ‘usiende sasa, si unaona namaliza hii.’

“Nikuongeze anti?” mhudumu alimuuliza kwa sauti iliyojaa mshangao mkubwa. Mama Pilima alikubali kwa kutingisha kichwa.

Hata hivyo, kuondoa usumbufu alimwambia amletee mbili kabisa.

“Du! Kweli wanawake wengine ni balaa… yaani huyu dada kaikata bia yote tena ya baridi bila kupumzika? Hii ni hatari!” yule mduhumu aliwaza.

Mhudumu alipoondoka, mama Pilima akamwangalia yule mwanaume na kusema…

“Sikukeri?”

“Wala!”

“Basi nashukuru sana…maana kuna watu wakikaa kwenye meza kama hivi wanapenda kukaa wenyewe tu.”

“Mimi wala,” alirudia kusema yule mwanaume…

“Oke, mimi naitwa Keti au mama Pilima…mwenzangu?” alianza kujitambulisha mama Pilima hata bila ya kuombwa…

“He! Kweli ndiyo jina lako?” alishtuka yule mwanaume…

“Ndiyo! Kwani vipi?”

“Mimi mke wangu pia anaitwa Keti lakini yeye ni mama Pili…”

“Mh! Hayo kweli maajabu! Ilikuajekuaje mpaka kufanana majina yetu na ya watoto?” aliuliza mama Pilima…

“Ndiyo nashangaa.”

“Kwa hiyo wewe ni baba Pili..?”

“Eee baba Pili!”

“Unaitwa nani ukiachana na jina la mwanao la baba fulani..?”

“Mimi naitwa Sam…”

“Hamna bwana,” alisema yule mwanamke huku akisimama na kuweka glasi ya bia mezani…

“Hamna nini sasa?”

“Yaani mimi nifanane majina na mkeo, wewe ufanane na mume wangu! Inawezekana kweli?”

“Kwani mumeo naye anaitwa Sam?”

“Eee! Ndiyo nashangaa hapa…”

“Mh! Hiyo kweli kali. Si ajabu hata makabila mimi na mumeo ni sawa?”

“Inawezekana baba Pili. Wewe kabisa gani?”

“Natoka Mkoa wa Dodoma…”

“Unaona sasa baba Pili…na mimi Sam mwenzako anatoka mkoa huohuo? Mkeo je?”

Baba Pili aliachia tabasamu na kusema…

“Aaa! Haiwezekani na wewe ukafanana kabila na mke wangu bwana. Itakuwa too much sasa!”

“We nitajie…wewe unatoka Mkoa wa Dodoma, mume wangu pia hukohuko. Je mkeo anatokea mkoa gani?”

“Yeye mke wangu anatokea Mkoa wa Dodoma pia…”

“Noo! Noo! Napingana  na wewe baba Pili. Kinachoonekana hapa kuna kitu unakitengeneza…”

“Kwa nini? Kwani mimi nakujua wewe?”

“Inawezekana unanijua kiroho au kimwili,” alisema mama Pilima akiwa amesimama bado tangu aseme zile noo zake!

“Mimi sijawahi kukuona hata siku moja. Lakini jua Mungu ana makusudi yake mama Pilima. We fikiria ni kwa nini ulikuja kuomba kiti kwangu? Halafu ukakosa pa kukiweka ukaja kukiweka hapahapa ulipokitoa?”

“Asee kweli kabisa baba Pili. Hapa nadhani pana neno tunaambiwa,” alisema mama Pilima…

“Eee! Nyie mnaishi wapi?” aliuliza baba Pili…

“Magomeni Kagera…”

“Ah! Nimechoka sana jamani…”

“Kwa nini?”

“Sisi  tunaishi Magomeni Mwembechai!”

“He! Kwa hiyo wote ni Magomeni?”

“Ndiyo maana yake.”

“Watoto wako wanasoma wapi?”

“Watoto mtoto? Mimi nina mtoto huyohuyo mmoja tu…”

“Aaa! Noo bwana…nooo!”

Je, nini kilitokea?

Usikose kusoma kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.

Comments are closed.