Baba wa Kagere Aibuka Dar, Ataka DNA -Video

ANAYESEMEKANAkuwa baba wa nyota wa Klabu ya Simba, Meddie Kagere, Vedasto Katologi ameibuka na kusema yeye ni baba wa nyota huyo.

 

Katologi ameliambia Championi Jumamosikuwa, alimpata Kagere baada ya kuwa na uhusiano na mwanamke wa Burundi ambaye hamkumbuki lakini anafahamu kuwa ndiye aliyemzaa staa huyo wa Simba.

 

Aliongeza kuwa hakumbuki jina la mwanamke huyo ambaye ni mama wa Kagere ila alianza kuhisi kuwa nyota huyo ni mwanaye baada ya kujiunga na Klabu ya Simba.

Championi Jumamosiambalo lilizungumza live na Katalogi kwenye makazi yake Mbezi Makabe jijini Dar, alifunguka vitu kibao kuhusiana na ishu hiyo ambavyo vingine utavipata live kupitia Global TV Online.

 

“Baada ya Meddie kujiunga na Simba nilipata taarifa kutoka kwa watu mbalimbali wa soka kipindi hicho mimi nilikuwa sifuatilii sana michezo ila nilianza kuangalia kwa ajili ya mwanangu (Kagere).“

 

Nilimtafuta Kagere akaniambia atanitafuta na kunitumia hela ya nauli ili nije Dar tuonane ila amekuwa kimya hata nikimtafuta hajibu.“

 

Nilifanya juhudi za kutafuta nauli na kuja Dar ili kuonana naye ila zikashindikana nikaishia kumuona meneja wa Simba akaniambia kuwa Kagere amesema hana ndugu hapa Tanzania ndugu zake wote wapo Afrika ya Kusini.“

 

Ninachoomba Waandishi wa Habari wewe nisaidie mimi kuonana naye nataka kupima naye DNA, kama hatakuwa mwanangu ni sawa na nitakuwa nimeridhika kuliko kukaa na maswali mengi kichwani, mimi sina shida na mali zake nataka kijua ukweli tu.

MWANDISHI WETU,Dar es SalaamTecno


Toa comment