BABA WA NEYMAR ATUA BARCELONA

MABOSI wa Barcelona juzi walikutana na mwakilishi wa mshambuliaji wao wa zamani Neymar wakifanya naye mazungumzo ili arudi kwenye timu hiyo.

 

Neymar kwa sasa ni mchezaji wa PSG ambaye aliuzwa hapo na Barcelona na sasa anataka kurejea kwenye timu hiyo ya Hispania. Mara kwa mara mchezaji huyo amekuwa akisema kuwa hana furaha ya kubaki Ufaransa na awali iliaminika kuwa anaweza kujiunga na Manchester United.

 

Mabosi wa Barcelona walikwenda kwenye kambi ya Brazil hivi karibuni ambapo inaelezwa kuwa wanataka kukutana na mzazi wa Neymar pamoja na mwakilishi wake kwa ajili ya mazungumzo ya usajili wa mchezaji huyo.

 

Imeelezwa kuwa PSG wameshamruhusu mchezaji huyo kujiunga na timu yoyote ile ambayo ataona kuwa anaweza kupata furaha na inaweza kufi kia dau lake.

 

Hata hivyo, gazeti la Esporte Interativo, lilisema juzi kuwa baba yake Neymar na mwanasheria wao wameshatua nchini Hispania kwa ajili ya mazungumzo ya dili hilo. Hata hivyo, inaaminika kuwa usajili wa Neymar unaweza kuwa zaidi ya pauni milioni 200 kutoka PSG kwenda Barca.

‘MAHAKAMA’ YAIHUKUMU STARS KWA MATOKEO MABAYA AFCON!


Loading...

Toa comment