The House of Favourite Newspapers

Baba wa Vincent Kompany Awa Meya wa Kwanza Mweusi Ubelgiji

 Pierre Kompany, right, at his son's bar in Belgium

UBELGIJI imechagua meya wa kwanza mweusi kwa mara ya kwanza.  Mtu huyo ni baba wa mwanasoka wa kimataifa Vincnt Kompany aitwaye  Pierre Kompany.

Kompany aliyeingia nchini Ubelgiji mwaka 1975 akiwa mkimbizi kutoka nchi ambayo sasa inaitwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, anakuwa meya wa manispaa ya  Ganshoren.

Kompany alijikita katika siasa akiwa diwani tangu mwaka 2006, na baadaye kupata ubunge katika jimbo moja jijini Brussels mwaka  2014.   Lakini huenda umaarufu wake unatokana na mwanaye ambaye ni mchezaji na nahodha wa klabu ya Manchester City ya Uingereza iliyoko kwenye ligi kuu ya nchi hiyo, na pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgji.

Kaka yake Vincent aitwaye, Francois, naye hucheza soka na klabu ya KSV Roeselare ya Ubelgiji.

“Baba yangu ni meya wa kwanza mwesi wa Ubelgiji, haijawahi kutokea katika historia, hongera baba yangu!” aliandika Vincent kwenye akaunti yake kwenye mtandao wa  Instagram.

 Kompany has won the Premier League three times with Man City

Comments are closed.