Kartra

Babu Alia: Mke Wangu Amenikimbia Kisa Ulemavu na Umaskini – Video

MZEE Matata mkazi wa Hai mkoani Kilimanjaro ambaye mwezi Januari, mwaka huu alipata ajali mbaya ya gari na kusababisha ulemavu wa mguu na kubadili kabisa ndoto za maisha yake na kujikuta katika hali ya ufukara.

 

Mzee Matata ameeleza kuwa hata mke wake amemkimbia sababu ya ufukara na anaomba Watanzania wamsaidie kwa sababu hali ya maisha yake ni mbaya sana na hana msaada.

 

“Mpaka sasa sina uwezo wa kufanya kazi yoyote ile sababu ya ulemavu wangu, nilipopata ajali nilivunjika mguu mara nne nikapelekwa KCMC baadaye nikarudishwa nyumbani, lakini mguu uliunga vibaya, hali yangu sio nzuri sina hata pesa ya matibabu, nimebaki kuombaomba tu misaada.

 

“Mama yao ameondoka ameenda kwao Mwanga, alitoka kama anakwenda kuchuma mboga akaondoka moja kwa moja, na wameniambia hawezi kurudi tena mpaka mwezi Desemba kama nitakuwa nimepata angalau pesa ili asiwe anachuma mboga. Hii ni mara ya pili, ananikimbia kwa sababu ya ufukara.

 

“Watoto wangu wanapata shida sana wakati mwingine hawaendi kabisa shule sababu ya njaa, hakuna chakula. Mwenye miaka sita ndiye angalau anapika lakini chakula ni kama cha kumpa mbwa, wakati mwingine kibichi lakini tutafanyaje, tunakula hivyo hivyo,” qamesema Mzee Matata.

 


Toa comment