The House of Favourite Newspapers

Babu Anaswa na Denti Live, Akiona cha Moto

DAR ES SALAAM: DUNIANI kuna mambo! Babu mmoja aliyejulikana kwa jina la Dotto, mkazi wa Kitangini Kata ya Chanika jijini Dar, amekumbwa na aibu ya mwaka na kukiona cha moto baada ya kunaswa kwenye jumba bovu na denti wa kidato cha kwanza (shule na jina lake tunalihifadhi) akidaiwa kutaka kuvunja naye amri ya sita.

 

Chanzo makini kililieleza Amani kwamba babu huyo alinaswa hivi karibuni baada ya kuwekewa mtego ambapo alinaswa akiwa kwenye jumba hilo ambalo halijaisha akitaka kufanya mapenzi na mwanafunzi huyo.

Kufuatia sakata hilo Amani lilifunga safari mpaka eneo la tukio na kuonana na mjumbe wa nyumba 50 wa shina namba 27 Mtaa wa Tungini, Barakati Selemani ambaye alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

 

Akizungumza mjumbe huyo alisema;

“Siku ya tukio majira ya saa mbili usiku mtuhumiwa alipita hapa nyumbani kwangu na baiskeli lakini ilipofika saa tatu kasoro usiku nikashangaa kusikia mayowe watu wakisema piga huyooo….piga huyo kazoea.”

Mjumbe aliendelea kueleza kuwa alipojaribu kufuatilia sauti hizo ndiyo akabaini kuwa walikuwa wakienda nyumbani kwake kumpelekea mtuhumiwa kama mjumbe.

 

“Walimfikisha mtuhumiwa hapa nyumbani kwangu huku chini akiwa mtupu amebaki na nguo za juu tu.

“Nilipowauliza amefanya nini wakaniambia wamemkuta kwenye nyumba ambayo haijaisha akitaka kufanya mapenzi na mwanafunzi, niliwauliza alipo huyo mwanafunzi wakanionesha binti ninayemfahamu ambaye naye ilisemekana kwenye hilo jumba hakuwa na nguo ila alipewa nafasi ya kuvaa baada ya kunaswa,” alisema mjumbe.

 

Baada ya hapo mjumbe huyo akawahoji ambapo alimuona baba wa huyo binti ambaye pia anamfahamu kwa jina la Rajabu naye akamuhoji ilivyokuwa ambapo alimwambia aligundua kuwa binti yake ameanza mchezo mchafu na mzee huyo hivyo siku hiyo waliwavizia kwa kujibanza kichakani na kufanikiwa kuwanasa.

Mjumbe alisema baada ya kuchukua maelezo hayo aliwasihi wananchi wasimdhuru yule mzee ambapo alifanikiwa kumpeleka Kituo cha Polisi Chanika ambapo aliwapa maelezo.

 

Baada ya maelezo hayo mjumbe pamoja na mashuhuda wa tukio hilo walimpeleka mwandishi kwenye jumba waliponaswa wawili hao na alipokuwa akiishi babu huyo. Ili kuleta usawa wa habari, mwandishi wetu alimfuata baba wa denti huyo ili azungumze machache kuhusiana na tukio zima lakini alikataa kutoa ushirikiano akidai kuwa anaogopa kuvuruga upelelezi wa kesi.

 

Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni, ilielezwa kuwa babu huyo alikuwa ameshikiliwa katika Kituo cha Polisi Chanika. Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Ilala, Ernest Matiko kuhusiana na tukio hilo, alisema halijafika kwenye dawati lake hivyo atalifuatilia na endapo itabainika lipo na mtuhumiwa anastahili mashtaka basi atafikishwa mahakamani.

Stori: Richard Bukos, Amani

Comments are closed.