The House of Favourite Newspapers

Babu Miaka 71 Anaswa na Vyeti 240, Mihuri 159 – Pichaz

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali  240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.

 

 

Nyaraka zilizo kamatwa ni pamoja na Vyeti vya kuzaliwa ,vyeti vya ndoa ,vyeti vya ubatizo, vyeti vya Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pamoja na mihuri mbalimbali miongoni mwao ikionyesha ni ile inayotumika wakati wa usajili vizazi na vifo katika manispaa ya Moshi na Kitete mkoani Tabora.

 

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa alisema vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya kuandikia (Type Writer) na kifaa cha kuwekea namba huku akiwataja watuhumiwa kuwa ni pamoja na Athuman Selemani (71) anayetajwa kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa wilaya.

 

Wengine ni Justine Mziray (55) anayetajwa kuwa ni mtaalamu wa kuchonga mihuri,Sporah Daud anayetajwa kushiriki katika uandaaji wa nyaraka hizo kwa kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu (Type writer) na Costa Lyatuu  anayetajw kuwa mtaalamu wa kughushi sahihi.

Comments are closed.