Babu Njenje Afariki Dunia

Taarifa iliyotufikia asubuhi hii inaeleza kuwa, mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro maarufu kama Wana-Njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo Mei 24, 2020 jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mmoja wanamuziki wa bendi hiyo, John Kitime amesema; “Ni kweli Babu Njenje amefariki dunia na sasa naelekea pale alipokuwa akiishi, Mtaa wa Mindu-Upanga ambapo taratibu zitafanyika.”
Babu Njenje atakumbukwa kwa nyimbo zake nyingi zikiwemo Njenje na Kinyaunyau. Kwa niaba ya Kampuni ya Global Publishers nasema Mungu ailaze roho ya Babu Njenje mahali pema peponi. Amina.
Na Sifael Paul

