Babu Tale Asimulia Usiyoyajua Kifo Cha Ombeni ‘’Alijisogeza Kwa Mungu Mapema’’ – Video

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamisi Taletale anaejulikana kwa jina maarufu Babu tale amehudhuria mazishi ya marehemu Ombeni na kusema kuwa kifo ni fumbo yeyote anaweza kutangulia kwa mwenyezi Mungu wakati wowote na kuongeza marehemu alikuwa mpole na mtumishi wa kiroho.
Ombeni alikuwa mtangazaji wa kituo kimoja cha Television ambapo leo amezikwa katika makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam, Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi.