The House of Favourite Newspapers

BABU WA GAMBA: “Bora Ningekufa Mimi, Nilimwandalia Urithi” – Video

Katika hali ya Majonzi, Babu wa Marehemu Isaac Gamba (92), anayeitwa Wilson Biseko Nyagabona, amezungumza kwa uchungu mkubwa juu ya kifo cha mjukuu wake huyo na namna ambavyo walikuwa wakipendana kiasi cha kufikia kumuandikia urithi wa mali zake na kwamba bora angekufa yeye Gamba akabaki kwa sababu alikuwa bado ni kijana ambaye nguvu zake zilihitajika kulijengza taifa

 

“Nimelazimishwa kusema wakati Isaac Nyagabona Gamba Muyenjwa akiwa kwenye jeneza, kifo cha huyu kijana kinanimaliza kabisha maisha yangu, wanapotaja sifa zake mimi naugua, ilikuwa ni haki kweli huyu kijana mdogo Isaac afariki dunia sasa hivi wakati na sisi wazee tupo?

 

“Wakati naandika urithi niliwaambia wanangu nikifa mtu wa kwanza kumpa taarifa awe mjukuu wangu wa Ujerumani, Isaac, na katika wajukuu huyu ndiye alikuwa wa kwanza kumwandikia urithi wa vitu vyangu. Sikutaka nife kienyeji watu waanze kugombania mali, ilikuwa ni haki kuandika kila kitu kabla sijazeeka sana na mikono ikashindwa kuandika,” alisema Mzee Nyagabona.

BABU WA GAMBA: “Bora ningekufa Mimi, Isaac Nilimuandikia Urithi”

Comments are closed.