The House of Favourite Newspapers

Baby Madaha ajiachia na bwana Dubai

0

Madaha1.jpg

Gladness Mallya
STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Madaha amedaiwa kupata mchumba ambaye ni mfanyabiashara wa mafuta mwenye asili ya Kiarabu anayefanya mishe zake Dubai na sasa wanakula zao ‘happy’ pande za huko.

Chanzo makini kililitonya Ijumaa kwamba, Madaha amekuwa ni mtu wa kusafiri kwenda Dubai mara kwa mara kwa sababu ya mtu wake huyo ambaye anampa jeuri ya pesa kwa sasa.

“Madaha ana bwana huko Dudai na ndiyo maana mara kwa mara anakwenda, jina la huyo mtu wake silijui ila ana asili ya Kiarabu,” kilidai chanzo.

Alipotafutwa Baby Madaha kwa njia ya Mtandao wa What’s App alikiri kuwepo Dubai na mpenzi wake huyo ila akasema sasa hivi hawezi kumzungumzia zaidi kwani ndiyo kwanza ‘wamelianzisha’.

Leave A Reply