Baby Madaha arejea na mbwembwe!

madahaGladness Mallya

BAADA ya kula bata kwa mwezi mmoja huko Dubai anakodaiwa kuwa pamoja na mfanyabiashara tajiri wa mafuta, msanii wa muziki na filamu Bongo, Baby Madaha amerejea kwa mbwembwe, akisema anajiandaa kufungua kampuni.

Akizungumza na gazeti hili, Baby Madaha alisema anatarajia kufanya uzinduzi wa kampuni hiyo ambayo pamoja na mambo mengine, itashughulika na filamu.

“Hapa ninapozungumza na wewe nipo bandarini nachukua vifaa nilivyonunuliwa na mpenzi wangu huko Dubai na baada ya zoezi hili nitarudi huko kwani ndipo yatakuwa makazi yangu makubwa,” alisema Baby Madaha.


Loading...

Toa comment