The House of Favourite Newspapers

Baharia wa Manzese

Ingawa kazi yake rasmi ilikuwa ni kusafisha na kutengeneza kucha mitaani, alifanya kila kazi iliyomjia mbele yake. Alibeba mizigo, alizoa taka majumbani mwa watu, alichota maji na kuwauzia wateja wake na kazi nyingine nyingi!

Yeye alichojua ni mkono uende kinywani! Alikuwa mchakarikaji kwelikweli. Sababu hiyo ndiyo iliyomfanya ajulikane zaidi kwa jina la Baharia!

Yes! Baharia wa Manzese!

Ni Baharia wa Manzese kwa sababu aliishi uswahilini kabisa, eneo la Manzese- Midizini. Alikuwa maarufu sana mitaani kutokana na tabia yake ya kupenda kujichanganya na kufanya kila kazi.

Huyu ni Sudi.

Sudi Maulid.

Pamoja na kujichanganya kote huko kwenye kila kazi, hata zile zilizoonekana ngumu na mbaya ambazo zisingeweza kufanywa na mabishoo wengi wa town. Sudi alikuwa handsome wa nguvu. Sifa hiyo ndiyo iliyosababisha aingie kwenye migogoro kila kukicha na washkaji wa mtaani kwao kwa hofu za kuwang’olea totozi zao.

Sudi hakujali, alishika hamsini zake, akipambana na changamoto hizo kila uchwao. Uzuri alikuwa mtu wa mazoezi. Pamoja na mikwara mizito aliyokuwa akikutana nayo, jamaa zake walikuwa wakihenya kutokana na nguvu alizokuwa nazo.

Leo ameamka asubuhi na mapema, amepeleka maji kwa mama Stella kisha amekwenda kubeba taka kwenye baa moja ya mtaani kwao, halafu akajiandaa, akachukua kapu lake lililokuwa na mazagazaga ya kutengenezea kucha, akaingia zake mitaani.

Kapu lilikuwa na kila kitu. Rangi za kucha, mashine za kukata kucha, msasa wa kusafisha, kucha za kubandika na vikorombwezo vingine vyote.

Baharia akazama mtaani kuendelea kusaka riziki!

***

“Sawa mpenzi, ila usisahau kuniletea kile kitu!”

“Kitu gani?”

“Asubuhi nilikuambia nini mpenzi wangu? Yaani mara hii tayari umeshasahau?”

“Nikumbushe bwana!”

“Sikukumbushi, kama utaleta niletee na kama hutaleta basi, lakini sitakukumbusha kabisa.”

“Sasa nitaota mpenzi wangu?”

“Nimesema sitaki!”

“Nina bwana baby, mbona unakuwa hivyo, niambie basi ni nini?”

“Kweli kama hukumbuki basi!”

“Sikia nikuambie Nina wangu, leo ni mara ya mwisho, nikumbushe kwa mara ya mwisho, nakuahidi siku nyingine nitakuwa makini, sitakuwa msahaulifu tena mpenzi wangu!”

“Kweli?”

“Nakuahidi Nina wangu!”

“Kweli Bebeto my love?”

“Sure! Niamini mimi mpenzi.”

“Haya, nakukumbusha… aaaashii…. mhmhm, sikia Bebe!” Nina

alipotaka kusema, akajikuta akianza kulalamika kimahaba kwenye simu.

Bebeto alichanganyikiwa, maana ilikuwa ghafla sana na hapakuwa na neno lolote alilolizungumza ambalo lingesababisha Nina atoe mguno ule.

“Wewe una nini? Hiyo miguno ni ya nini?”

“Mh! Mh! Mh!” Nina akabaki kuguna zaidi.

“Nina!”

“My Bebe!”

“What is wrong with you? Mbona sikuelewi?”

“Nothing honey!”

“Unatania.”

“Hakuna Bebe.”

“Ok! Nikumbushe.”

“Usisahau kuniletea chocolate, sawa mpenzi wangu?”

“Ok!”

“Bye… aaaashiiiii….” Nina alivyokuwa akiaga bado aliendelea kulalamika.

“Lakini una nini?” Bebeto akauliza tena.

Nina hakujibu.

Akakata simu.

Kilichofuata baada ya kukata simu ni kuangua kicheko cha nguvu kisha akayatuliza macho yake kwa kijana mtanashati aliyekuwa mbele yake akihangaika kusugua kucha zake kabla ya zoezi la kupaka kucha rangi kuanza.

Kelele za miguno alizokuwa akipiga Nina, zilisababishwa na jinsi kijana huyo alivyokuwa akimsugua kucha kimahaba. Alikuwa

Sudi!

“Vipi mbona ulikuwa unamfanyia hivyo shemeji? Vibaya hivyo!” Sudi akamwambia Nina akitabasamu.

“Bwana wangu… unafikiri ni kwa hiyari yangu basi? Nimejikuta nikipagawa na jinsi unavyonitekenya. Na wewe kwa sifa sasa, ndiyo ukawa unazidisha!”

“Acha utani, kwa hiyo nakutekenya sana?”

“Yaani we acha tu, umenichanganya sana anko Sudi.”

“Kama nini?”

“Kama nipo chumbani na shemeji yako, lakini inaonekana una manjonjo wewe…” Akasema Nina kwa sauti ya kimahaba.

“Umejuaje?”

“Nimejua tu.. aaash… Sudi bwana, taratibu.”

Nina alishachanganywa na utundu wa Sudi. Tayari hisia zake zilishahama na alitamani sana kama ingewezekana angekuwa faragha na kijana huyo mtanashati anayevutia.

“Twende ndani Sudi, hapa nje sipo comfortable kabisa.”

“Poa!” Sudi akajibu akikusanya vifaa vyake kwenye kapu, akijiandaa kuingia ndani.

Tayari Nina alikuwa ameshatangulia ndani. Kitambo kidogo, Sudi akainuka na kuanza kupiga hatua kuelekea ndani. Alipofika sebuleni, akasikia sauti ya Nina ikimwambia; “Njoo huku chumbani usiogope.”

Sudi bila kusita akaingia, alichokutana nacho, kilimshangaza sana. Ilikuwa kidogo aanguke. Nina alikuwa mtupu kama alivyozaliwa, macho yake ameyalegeza utadhani ametoka kula kungu!

“Sudi please, maruhani yangu yameshapanda, tayari yatulize,” Nina akasema kwa sauti laini na tamu kuliko kawaida.

Sudi akabaki ameyatoa macho yake kwa mshangao mkubwa. Ghafla kapu lake likadondoka chini. Akiwa bado anatahamaki, Nina akaanza kupiga hatua kumfuata. Udenda wa mahaba ukaanza kumtoka Sudi.

***

Baada ya Bebeto kukata simu ya mpenzi wake Nina, hakuwa na amani kabisa, alihisi lazima kuna mjanja alikuwa anamlia mali zake. Haikuwa sauti ya mpenzi wake aliyoizoea. Ndiyo… wakati mwingine alikuwa akiisikia, lakini chumbani tu.

Aliingiwa na shaka sana!

“No! Siwezi kuwa mjinga wa kiasi hiki, ngoja niende nyumbani…” Bebeto akajisemea moyoni mwake, akizima kompyuta yake na kutoka zake nje ya ofisi.

Alikuwa anakwenda nyumbani!

Kama mbwai mbwai!

***

Alihisi kama mwili wake umekufa ganzi, kuna wakati alikuwa akidhani huenda alikuwa yupo ndotoni tu! Sudi alichanganywa

sana na uzuri wa Nina, mwanamke ambaye alikuwa anavutia kuliko kawaida. Bado amesimama anamtazama kwa woga huku akiwa hajui la kufanya.

Midomo ya Nina ikaanza kucheza kimahaba, macho yake yakizidisha rangi nyekundu, kama ambaye alikuwa ametoka kulala kama siyo kulia muda mfupi uliopita.

Lakini kubwa zaidi liliomuacha hoi ni ile hali ya macho yake kuwa malegevu kama ameelemewa na usingizi mzito!

Itaendelea wiki ijayo.

 

Amrani Kaima

Maoni/ushauri simu: +255 658 798787

Comments are closed.