Bahati Nasibu Ya Shinda Gari Ilivyotikisa Tabata Mawenzi

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam (kulia) akiwafafanulia jambo wasomaji wa magazeti ya Championi na Spoti Xtra juu ya namna ya kushiriki bahati nasibu ya Gari.

Wasomaji wakiendelea kupatiwa ufafanuzi.

Bahati Nasibu ya shinda gari  iliyopewa jina la Chomoka na Gari Mpya  inayopatikana kupitia magazeti ya Championi na Spoti Xtra ambapo wasomaji wa magazeti  wa maeneo ya Tabata Mawenzi  jijini Dar es Salaam wameendelea kufunguka juu ya wanavyoendelea kununuana kukata kuponi kwa ajili ya kuingia katika droo hiyo.

 

 

 Kama kawaida maofisa masoko wa Global Publishers walitembelea maeneo hayo na kushuhudia umati wa watu wakijaza kuponi  kwa ajili ya kuingia katika droo ya bahati nasibu hiyo ambayo mshindi atanyakua ndinga mpya aina ya FunCargo.

 

 

Akipiga stori na wasomaji hao Ofisa Masoko wa Global Publishers, Anthony Adam,  amewasisitiza wananchi hao kununua kwa wingi magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili waweze kuwa miongoni mwa washindi.

 

‘Niwasihi wakazi wa Kigamboni muendelee kununua magazeti yetu ili muwe miongoni mwa washindi, tutatoa gari mpya siku ya mwisho ya droo na kabla ya droo kubwa wapo ambao kila wiki watakuwa wanajinyakulia simu mpya za kijanja, Smart Kitochi, ambazo ndani yake kutakuwa na bando la bure na APP ya Global Radio.

 

JINSI YA KUTUMA:

Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza-Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie GariGlobal PublishersS.L.P 7534, Dar es Salaam.

Kwa maelezo zaidi, piga simu no: 0717 020792 au 0672 324759.

 

 

MASHARTI YA KUSHIRIKI:

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.

 

 

Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

 

Toa comment