‘Shinda Gari’: Wasomaji Vingunguti Wajaza Kuponi Kibao – Video
MAPEMA leo Jumatano, Aprili 29, mwaka huu timu ya maofisa masoko ya Kampuni ya Global Publishers ilitembelea maeneo ya Vingunguti na maeneo mengine ya jijini Dar es Salaam ambapo wadau wa wamelichangamkia Gazeti la Championi Jumatano.
Akizungumza baada ya ziasa hiyo fupi, Mkuu wa Idara ya Usambazaji ya Global Publishers, Anthony Adam alifunguka kuwa droo ya tatu ya bahati nasibu ya jishindie gari na Championi na Spoti Xtra inatarajia kufanyika wiki ijayo.
Adam amesema wanaangalia uwezekano wa kuboresha droo hiyo ya tatu ikiwemo ishu ya zawadi na idadi ya washindi ambao watapatikana kutoka katika droo hiyo wanaweza kuongezeka maradufu.
Mpaka sasa jumla ya washindi tisa wamepatikana kupitia droo mbili zilizochezwa, droo ya kwanza ilitoa washindi watatu ambao walizawadiwa simu janja, huku washindi sita wa droo ya pili wakizawadiwa fedha shilingi 50,000.
Mbali na hilo Anthony alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza wasomaji wa Championi kuendelea kulisoma gazeti hilo na kutoipuuzia bahati nasibu hiyo iliyopea jina la Baba Lao kwa kuwa ni kweli inatoa washindi.
“Yapo makundi ya watu ambao ni wasomaji wazuri wa gazeti letu la Championi, lakini wamekuwa na imani ndogo na bahati nasibu yetu, wanahisi kuwa bado kuna ujanjaujanja unafanyika.
“Nitumie nafasi hii kuwaomba na kuwasisitiza kuwa, watu wanaondoka na zawadi kupita droo hizo ndogondogo, pia ni kweli gari mpya yenye thamani ya Sh milioni 10, itatolewa kwenye droo kubwa.
“Watu wanavuna zawadi kupitia droo zetu ambazo tunazichezesha kila mara, wajaribu kujaza kuponi katika ukurasa wa pili wa Gazeti la Championi na wataona matokeo yake,” alisisitiza Anthony.
JINSI YA KUSHIRIKI
Nunua Gazeti la Championi, kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.
JINSI YA KUTUMA:
Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.
MASHARTI YA KUSHIRIKI:
Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.
Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi. Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.






