The House of Favourite Newspapers

Shinda Nyumba Yawafikia Wakazi wa Bunju na Boko

0

Mkazi wa Bunju Peter Mwita akipata maele-001Mkazi wa Bunju, Peter Mwita (kulia) akipewa maelekezo muuzaji wa Magazeti ya Global Publishers, Khadija  jinsi ya kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba. Mkazi wa Boko Musa rajabu akijaza kopon yake-001Mkazi wa Boko, Mussa Rajabu akijaza kuponi ya Shinda Nyumba mara baada ya kununua Gazeti la Uwazi Jumanne. Mkazi wa bunju akipata maelekezo ya namna ya kujaza kuponi yake kutoka kwa Afisa promosheni Jimmy Haroub-001Afisa Promosheni, Jimmy Haroub (katikati) maelekezo kwa msomaji wa Magazeti ya Global Publishers namna ya kujaza kuponi na kushiriki Shinda Nyumba. Mkazi bunju akinunua gazeti kutoka w muuzaji wa Global publishers-001Mkazi Bunju akinunua Gazeti la Uwazi. Salum telelomkaziwa Boko magengeni akiwana afisa masoko Yohana Mkanda-001 Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Yohana Mkanda akitoa maelekezo kwa Mkazi wa Boko Magengeni, Salum Telelo namna ya kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

Sevelina Julias mkazi wa Boko magengeni akivalishwa zawadi ya kofia na afisa masoko Yohana Mkanda-001Mkazi wa Boko Magengeni, Sevelina Julius akipewa zawadi ya kofia na Ofisa Masoko, Yohana Mkanda.Aisha Bakari mkazi wa Boko magengeni akinunua gazeti kutoka kwa muuza magazeti wa Global publishers-001Mkazi wa Boko Magengeni, Aisha Bakari akinunua Gazeti la Uwazi Jumanne ili ashiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

IKIWA ni mara ya kwanza Bahati Nasibu inayoendelea kutikisa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar na maeneo mengine ya mikoa ya Tanzania, jana ilionekana kutua Bunju na Boko Jijini Dar, ambapo wakazi wa maeneo hayo walionekana kuvutiwa nayo baada ya kujitokeza kwa wingi kuchangamkia magazeti ya Kampuni ya Global Publishers Ltd kwa kuyanunua na kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu hiyo.

Mara baada ya maofisa wa Global Publishers, Yohana Mkanda na Jimmy Haroub kutua maeneo hayo wasomaji wa Gazeti la Uwazi walijitokeza kwa wingi na kununua gazeti hilo kisha kujaza kuponi zinazopatikana kwenye ukurasa wa pili katika gazeti hilo huku pia wakijipatia zawadi za kofia zenye nembo ya Shinda Nyumba zilizokuwa zikitolewa.

Akizungumza na wakazi wa maeneo hayo Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda alisema: “Wanachotakiwa kufanya wakazi wa Boko na Bunju na maeneo mengine ni kununua magazeti ya Global na kujaza kuponi zinazopatikana ndani ya magazeti ambayo ni Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Ijumaa Wikienda, Amani, Risasi Jumamosi na Ijumaa ambayo huuzwa kwa shilingi mia tano na msomaji anaweza kujishindia nyumba ya kisasa, kila anayejaza kuponi nyingi anajiongezea nafasi ya kujishindia nyumba na zawadi nyingine,”

“Bahati nasibu hiyo in aendelea nchi nzima, hivyo ni fursa kwa Watanzania wote na wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers kushiriki shindano hilo kwani yeyote anaweza kuibuka mshindi wa nyumba hiyo.” Alisema Mkanda.

PICHA NA YASSIN MAGANGA/GPL

Leave A Reply