Bahati Nasibu ya Taifa na Posta Washirikiana Kupanua Upatikanaji wa Michezo ya Kubahatisha
Dar es Salaam, 20 Machi 2025 – Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania inayo furaha kutangaza
ushirikiano wa kimkakati na Shirika la Posta Tanzania, wenye lengo la kuongeza upatikanaji wa
michezo ya kubahatisha kote nchini.
Kupitia ushirikiano huu, majukwaa ya Bahati Nasibu ya Taifa yatapatikana katika ofisi 207 za Posta, hatua itakayorahisisha upatikanaji wa michezo ya kubahatisha kwa Watanzania wanaoishi mijini na vijijini.
Kupitia mtandao mpana wa Shirika la Posta, wenye jumla ya ofisi 430 zinazotoa huduma kwa
watu 79140 kwenye kila kituo, Mtandao huu utatoa jukwaa madhubuti kwa Bahati Nasibu ya
Taifa kufanikisha azma yake ya kuwafikia Watanzania wote.
Kwa kuunganisha majukwa ya bahati nasibu katika vituo hivi, Bahati Nasibu ya Taifa itahakikisha hata wale wanaoishi maeneo yasiofikika kwa urahisi wanapata fursa ya kushiriki katika michezo hii.
Akizungumza wakati wa utiaji saini baina ya pande hizi mbili, Kelvin Koka, Mkurugenzi wa
Ithuba Tanzania,Amesema:
"Ushirikiano na shirika la posta Tanzania ni hatua kubwa sana ya dhamira yetu ya kuhakikisha
kuwa kila mtanzania anaweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha.
Kwa kutumia mtandao mpana na wakuaminika wa shirika la posta, tutafanikiwa kuwafikia watu wote nchi zima, na kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kushiriki katika michezo ya kubahatisha. Hivyo basi ushirikiano huu ni uthibitisho wa dhamira ya ujumuishi kwa maendeleo ya taifa.
Naye Constantine John Kasese, ambaye ni Mkurugenzi wa Biashara za Kielektroniki na Huduma
za Kifedha wa Shirika la Posta Tanzania, ameongeza kuwa:
" Sisi kama Shirika la Posta Tanzania, tumejikita katika kuwaunganisha watu na huduma
muhimu kote nchini. Ushirikiano baina yetu na Bahati Nasibu ya Taifa unawiana na maono yetu
ya kutoa huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu.
Kupitia upatikanaji wa majukwaa ya bahati nasibu katika ofisi zetu,Itasaidia kuleta urahisi wa upatikanaji wa tiketi za michezo ya kubahatisha na kuchangia juhudi za taifa za kuwainua wananchi wetu.
Kwa kutumia miundombinu madhubuti ya Shirika la Posta Tanzania, Jukwaa la Bahati Nasibu
ya Taifa linalenga kutoa michezo iliyo rafiki, rahisi, na yenye uwazi kwa washiriki wote,
ikiimarisha dhamira yake ya kuboresha maisha ya Watanzania kote nchini.
Kuhusu ITHUBA
ITHUBA ni mtoa huduma rasmi wa Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania, aliyeteuliwa kwa
kipindi cha miaka minane. Kama kiongozi wa michezo ya bahati nasibu barani Afrika, ITHUBA
inaleta utaalam na ubunifu wa hali ya juu nchini Tanzania, ikihakikisha uzoefu wa