Bajaji za Bei Chee Zamwagwa Dar, Wahi Uchukue Ya Kwako Kabla Hazijaisha – Video
Kampuni ya SEPCO Debt Collection and Auctioneering inakutangazia mnada mnada wa hadhara kwa idhini waliyopewa na Kampuni ya Wakazi Holding Group Ltd, watafanya mnada wa hadhara kwa kuuza bajaji kwa bei chee.
Mnada huo utafanyika Desemba 16, 2023 kuanzia saa 4:00 asubuhi katika ofisi zao zilizopo Tabata, mkabala na Kitambaa Cheupe. Ni bajaji ambazo ni nzima kuwasha na kuondoka. Unaweza kutumia kwa biashara ya mizigo ama kubeba abiria.
Ukaguzi wa bajaji hizo utafanyika kuanzia Desemba 12, 2023 hadi siku ya mnada kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 1:00 jioni katika ofisi za SEPCO zilizopo Tabata, jijini Dar es Salaaam.
MASHARITI YA MNADA
1. Mnunuzi atakayebahatika kununua bajaji atalazimika kulipa papo hapo asilimia 30 ya bei itakatokuwa imefikiwa, na asilimia 70 iliyobaki atalipa ndani ya siku 7 kuanzia siku ya mnada na akishindwa kulipa mnada utarudiwa na pesa aliyolipa awali haitarudishwa.
2. Mnunuzi atalazimika kuondoa bajaji aliyonunua mara baada ya kukamilisha malipo yote taslimu.
3. Gharama za kutoa bajaji alilonunua ni za mteja mwenyewe.
4. Bajaji itauzwa kama ilivyo na ukiharibu haitarudishwa
5. Kwa yeyote atakayeharibu mnada hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Kwa mawasiliano zaidi, fika katika ofisi zetu zilizopo Tabata karibu na Kitambaa Cheupe au piga simu namba 0715683777 au 0716535221.
Karibu chagua bajaji kwa bei chee ukapige hela mtaani.