Bajeti 2021/2022: Bodaboda, Bajaji Faini 10,000 Kutoka Sh30,000
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba leo Juni 10, 2021 akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya serikali ya Tanzania kwa mwaka wa fedha 2021/2022
“Napendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani sura 168 kwa makosa ya pikipiki na bajaji kutoka Sh30,000 za sasa hadi Sh10,000 kwa kosa moja. Lengo la hatua hii ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa. Aidha, adhabu kwa makosa mengine ya vyombo vya moto zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria zinaendelea kubaki kama ilivyo sasa,” amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba.