The House of Favourite Newspapers

Bajeti ya Serikali 2024/2025: Marufuku Kulipa Kwa Fedha za Kigeni – Video

0
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba

Serikali imeelekeza kuanzia Julai 1, 2024, wadau wote wa ndani, taasisi za umma, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika ya kimataifa na watu wote waliopo nchini Tanzania wenye tabia ya kuweka bei kwenye huduma au kuuza bidhaa kwa fedha za kigeni kuacha mara moja na kuhakikisha bei za bidhaa na huduma hizo zinatangazwa na kulipwa kwa Shilingi ya Tanzania.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha bungeni Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/2025.

Aidha amezielekeza taasisi zote za Serikali zinazotoza ushuru, ada na tozo mbalimbali kwa fedha za kigeni kurekebisha kanuni zao ili tozo hizo zilipwe kwa shilingi. Amesema hata mgeni akija na fedha za kigeni ni vyema akazibadilisha kuwa fedha ya Tanzania ili aweze kupata huduma.

“Tunafanya kila malipo kwa fedha za kigeni, halafu shilingi ikishuka thamani tunajiuliza tumekosea wapi,” ameeleza.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha bungeni Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2024/25.

Leave A Reply