BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) linatarajia kufanya mkutano utakaojadili hali ya mmomonyoko wa maadili unavyoathiri jamii nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata na msemaji wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Khamis Mataka, alisema mkutano huo utafanyika Aprili 24 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuwakutanisha mabalozi kutoka nchi mbalimbali, masheikh wa mikoa mbalimbali na watu wengine.
Na Denis Mtima/GPL