The House of Favourite Newspapers

BAKWATA yatangaza Juni 17, 2024 ni Sikukuu ya Eid el Adh’haa

0
Katibu Mkuu wa BAKWATA Taifa, Alhaji Nuhu Mruma.

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limesema, Sikukuu ya Eid el Adh’haa itakuwa Jumatatu ya Juni 17 na sala yake itaswaliwa katika msikiti wa Mohamed VI uliopo makao makuu ya baraza hilo Kinondoni.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 8, 2024 na Katibu Mkuu wa BAKWATA Taifa, Alhaji Nuhu Mruma.

Amesema,sala ya Eid itaanza saa moja asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid litakalofanyika pia katika msikiti huo.

“Kwa niaba ya BAKWATA, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir anawatakia maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” amesema Alhaj Mruma katika taarifa hiyo.

Eid El Adh’haa ni sikukuu inayoadhimishwa baada ya waumini wa Kiislamu kukamilisha ibada ya Hijja ambayo ni nguzo ya tano katika nguzo za dini.

 

Leave A Reply