Balaa! Mapokezi ya Carlinhos Yatetemesha Yanga – Video
KIUNGO fundi, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo ‘Carlinhos’ (25), amewasili rasmi nchini tayari kuanza majukumu yake ndani ya mabingwa wa kihistoria, Yanga SC, yenye maskani yake Mtaa wa Jangwani jijini Dar es Salaam.
Carlinhos ametua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mchana wa leo Agosti 25, 2020 akipokelewa na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said.
Mamia ya mashabiki wa Yanga wamejitokeza uwanjani hapo kumpokea na kumlaki mchezaji huyo ambaye ni raia wa Angola.
Carlinhos amezaliwa Machi 19, 1995, Luanda nchini Angola na alikuwa akiichezea timu ya GD Interclube Luanda kabla ya kujiunga na Wanajangwani.
Katika msimu wa 2019/2020, Carlinhos ameweka kambani mabao 11 katika game za ligi nchini humo.