Balozi Nchimbi Awasili Kufunga Kampeni za Serikali za Mitaa Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo tarehe 26 Novemba 2024, akiwasili katika Viwanja vya Kwamnyani, Mbagala wilayani Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, kwa ajili ya kufunga rasmi kampeni za Serikali za Mitaa kwa mkoa huo.
Ni mkutano wa mwisho kwa ajili uchaguzi wa viongozi wa vijiji, vitongoji, na mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 27 Novemba 2024, ambapo zaidi ya wapiga kura milioni 30 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo Tanzania Bara.