The House of Favourite Newspapers

Balozi Seif afanya usafi kwenye uzunduzi wa sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi

0


bb204693-1d7c-471d-9d76-01ac74437d55Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akishiriki na Wananchi, Vikundi ya vya usafi wa mazingira pamoja na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafi wa mazingira hapo Kwahani Uwanja wa Farasi ikiwa ni kuanza rasmi kwa maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

525bcae9-fe57-4209-9871-38101a107439Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira Mwenyekiti wa Kikundi cha Usafi wa Mazingira cha Kilimani { Kilimani City } Nd. Khamis Shaali Chum  { mwenye T. Shirt Nyeupe  }vilivyotolewa zawadi na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara ya Mazingira.Kushoto ya Mwenyekiti huyo wa Kilimani City ni Mkurugenzi Maingira Nd. Juma Bakari Alawi na wa kwanza kutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mazingira Zanzibar Nd. Juma Mjaja.

bf3f366a-c20e-42d8-97cc-1d2de0f4b500Baadhi ya wapiganaji wa Vikosi vya ulinzi wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira katika Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi kuanza kwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia Miaka 52. Picha na – OMPR – ZNZ.

3cc425c0-ee06-47ec-a347-a4fccfa90f54Watendaji wa Baraza la Manispaa Zanzibar wakijumuika pamoja na Wananchi na Vikosi vya Ulinzi kwenye usafishaji wa mazingira hapo Mtaa wa Kwahani Uwanja wa Farasi Mjini Zanzibar.

Leave A Reply