The House of Favourite Newspapers

BancABC Yatumia Milioni 18.9 Kukarabati Vyoo Dar Es Salaam Sekondari

0
Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Imani John akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

Dar es Salaam, 14 Desemba 2022: BancABC imetumia shilingi milioni 18.9 kukarabati vyoo vya Shule ya Sekondari Dar es Salaam iliyopo Ilala Gerezani jijini.

Awali shule hiyo yenye wanafunzi 635 ilikuwa ikitumia matundu kumi ya vyoo huku wakishirikiana na walimu uwiano ambao haukuwa mzuri kiafya.

Naibu Spika Mussa Hassan Zungu (mwenye kofia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa vyoo hivyo. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Gerezani, Fatuma Abubakar akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Imani John.

 

Baada ya BancABC kusikia kilio hicho iliwasiliana na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Naibu Spika Mussa Hassan Zungu ambaye aliwapa Baraka zote katika kuvifanyia ukarabati vyoo vilivyokuwa havitumiki ambapo ukarabati huo uligharimu milioni 18.9 na sasa kuwa na jumla ya matundu 37 uwiano ambao salama kiafya.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa vyoo hivyo mwakilishi wa mwalimu mkuu wa shule hiyo katika risala yake aliishukuru sana benki hiyo kwa kuwajali wananchi na kurejesha fadhila kwa jamii kwa kile wanachokipata ususan kuikumbuka shule yao.

Wageni waalikwa wakijionea vyoo hivyo.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC, Imani John amesema kitendo walichofanya ni kurejesha fadhila kwa jamii kutokana na kile wanachokipata na kubwa zaidi ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake na kuboresha elimu.

“Rais Mama Samia Suluhu Hassan amekuwa akipambania sana kuiboresha sekta ya elimu hivyo nasi tumeona tumuunge mkono kwa hili tulilolifanya.

Naibu Spika akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC kwa msaada wao huo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Gerezani, Fatuma Abubakar

 

Hata hivyo tunamuahidi kuendelea kumuunga mkono popote tutakapogundua kuna changamoto ambayo ipo ndani ya uwezo wetu.” Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC.

Kwa upande wake mgeni rasmi Mussa Hassan Zungu aliishukuru benki kwa kitendo hicho cha kiungwana kwa kutumia gharama hiyo kukarabati vyoo hivyo.

“Niwapongeze sana BancABC kwa msaada huu mkubwa wa kukarabati vyoo hivi vilivyokuwa havitumiki lakini sasa vimekuwa vya kisasa kabisa na maji yanatiririka vizuri kabisa.

“Nitumie nafasi kuwashauri wananchi nasi kufanya uzalendo kwa kuitumia benki hii ambayo inatoa huduma mbalimbali na masharti nafuu kabisa”. Alimaliza kusema Zungu na kuendelea na tukio la uzinduzi. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS GPL

Leave A Reply