Banda Ang’oka Baroka Aenda Kaizer

 

Mtanzania,anayeichezea Baroka FC Abdi Banda.

KWA mujibu wa Magazeti ya Afrika Kusini, beki Mtanzania,anayeichezea Baroka FC Abdi Banda ataondoka kwenye klabu hiyo muda wowote kuanzia Krismasi.

 

Habari za uhakika kutoka ndani ya Baroka ni kwamba Banda mwezi huu atajiunga na klabu moja iliyoko kwenye Jimbo la Gauteng Kaskazini mwa Afrika Kusini ambapo Spoti Xtra limebaini kwamba ni Kaizer Chiefs.

 

H a b a r i zinasema kwamba m a z u n g u m z o bado yanaendelea baina ya klabu hizo lakini tayari Baroka w a m e s h a n u n u a mbadala wa Banda ingawa yeye hajui lolote.

Banda akiwa na mke wake dada wa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’, Zabibu Kiba.

Banda alijiunga na Baroka ambayo haifanyi vizuri kwenye Ligi ya Afrika Kusini, mwaka jana akitokea Simba.

Amecheza mechi kadhaa kwenye klabu hiyo huku akisumbuliwa na majeraha, uongozi umesisitiza kwamba hauna mpango wa kubadilisha benchi la ufundi.

 

Mmoja wa viongozi wa Baroka amesema kwamba tayari wamemsajili Vusi Sibiya raia wa Afrika Kusini, mwezi uliopita kutoka Tshwane U n i v e r s i t y kuziba nafasi ya Banda.

“Tunaelewa kinachoendelea ndio maana t u m e a m u a kabisa kuziba nafasi yake kwa kutumia beki huyo chipukizi,” aliongeza kigogo huyo.

Loading...

Toa comment