The House of Favourite Newspapers

Banda: Dili la Sauzi Limetiki, Nasepa Zangu

0

STORI: Omary Mdose na Ibrahim Mussa | CHAMPIONI IJUMAA| DAR ES SALAAM

BEKI wa Simba, Abdi Banda, kwa sasa yupo huru kuendelea kuitumikia timu yake baada ya Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia mechi mbili ambazo tayari imeshapita.

Lakini habari nzuri ni kuwa Banda ameweka wazi juu ya dili lake la kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini kwa kusema msimu huu utakuwa wa mwisho kuichezea Simba baada ya hapo ataondoka kwenda kucheza soka la kulipwa.

Banda alipelekwa kwenye kamati hiyo kwa kosa la kumpiga ngumi, George Kavilla wa Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Aprili 2, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. Katika mchezo huo Simba ilifungwa 2-1.

Kamati hiyo iliyokaa juzi Jumatano kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya kaimu mwenyekiti wake, Jerome Msemwa, kosa alilolifanya Banda alitakiwa kufungiwa kati ya mechi tano mpaka kumi pamoja na faini ya shilingi milioni moja.

Kamati hiyo ilimpunguzia adhabu Banda kutokana na kuomba radhi kwa kitendo alichokifanya, ikumbukwe kuwa, kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Banda alisimamishwa na Kamati ya Saa 72 kutoitumikia Simba kutokana na kufanya kosa hilo, ambapo alizikosa mechi mbili dhidi ya Mbao FC na Toto Africans.

Kuhusu mazungumzo na timu ya Chippa United ya Sauz alisema: “Nilikwenda Afrika Kusini kuzungumza na Chippa United ambao waliniita kwa ajili ya mazungumzo na si kufanya majaribio, nilirudi Jumanne usiku.

“Sikutaka kwenda kufanya majaribio kwa kuhofia ningeweza kutibuana na viongozi wangu.

“Mkataba wangu na Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo msimu ujao nitaenda kuungana na Chippa tayari kwa ajili ya kuanza kuitumikia.”

Leave A Reply