Banda la Maliasili; Kivutio Kikubwa Sabasaba, Dar
Wananchi wakipita katika lango kuu la Viwanja vya Sabasaba jijini Dar na kukaguliwa.
Baadhi ya wananchi wakijipanga katika mstari kuingia viwanjani hapo.
Ulinzi ukiwa umejipanga vya kutosha.
Wananchi wakiendelea kukaguliwa.
Baadhi ya vivutio kwa watoto vilivyopo ndani ya viwanja hivyo.
Harakati za hapa na pale zikiendelea viwanjani hapo.
Jengo la maonesho ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika viwanja vya sabasaba.
Patson Asumwisye akiwapa maelekezo mbalimbali juu ya shughuli za Bunge baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye Banda la Bunge.
Ofisa Mawasiliano wa Bunge, Patson Asumwisye Sobha akizungumza na Global TV Online.
Banda la Chuo Kikuu Cha Muhimbili katika viwanja hivyo.
Jengo la Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika maonesho hayo.
Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar.
Baadhi ya wageni kutoka mataifa ya nje wakitazama mfano wa Mlima Kilimanjaro katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
Sanamu ya picha ya Simba katika banda la maliasili.
Meno ya Tembo yakiwa katika maonesho hayo.
Baadhi ya wananchi wakitembelea nyumba ya kabila la wazanaki.
Wananchi wakitazama samaki waliofugwa katika maonesho hayo.
Nyati akiwa katika maonesho hayo.
Wananchi wakiangalia Simba walioko katika maonesho hayo viwanja vya sabasaba jijini Dar.
Baadhi ya wananchi wakiangalia bustani za mbogamboga zilizolimwa na jeshi la magereza katika maonesho hayo.
Nyanya katika maonesho hayo.
Vitunguu katika maonesho hayo.
Shamrashamra za wananchi katika maonesho hayo.
BANDA la Wizara ya Maliasili na Utali lililoko katika Viwanja vya sabasaba limeonekana kivutio kuliko mabanda mengine baada ya kamera hii kunasa wananchi wakiingia kwa wingi kuona vivutio mbalimbali vilivyopo.
Mbali na banda la Wizara ya Maliasili na Utalii pia maonesho hayo yameonekana kuendelea kupamba moto sasa ikiwa ni siku ya kwanza kuzinduliwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Maonesho hayo ambayo ni ya 40 kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere eneo la Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam yana kauli mbiu ya Pamoja Tunaweza Kujenga Uchumi wa Nchi Yetu.
PICHA NA DENIS MTIMA / GPL