The House of Favourite Newspapers

Banda Mali ya Simba, Kashatua

0

UMAFIA!!! Ndivyo utakavyoweza kusema ni baada ya mabosi wa Simba kufanikisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa Big Bullets ya nchini Malawi, Peter Banda.

 

Hiyo ikiwa ni siku moja tangu zizagae tetesi za kiungo huyo kutekwa na mabosi wa Yanga kumficha na kumzimia simu kwa ajili ya kufanikisha usajili wake katika msimu ujao.

 

Championi ambalo ndiyo namba moja la michezo nchini, ndiyo lilikuwa gazeti la kwanza kuandika habari za kiungo huyo kutua kujiunga na Simba katika usajili wa sasa.

 

Mmoja wa mabosi wakubwa wenye ushawishi wa usajili ndani ya Simba, kimeliambia Championi Jumatano kuwa, kiungo huyo jana saa kumi kamili jioni alisaini mkataba wa miaka mitatu kisha akatambulishwa rasmi.

Bosi huyo alisema kuwa, kiungo huyo amesaini mkataba huo Goldeni Tulip Hotel,

Masaki jijini Dar es Salaam alipofikia mara baada ya kutua nchini akitokea Malawi ,Aliongeza kuwa, viongozi wa Simba ndiyo waliomtumia tiketi kiungo huyo ambaye hadi jana alikuwa akitajwa kusaini Yanga iliyokuwa inadaiwa kuwania saini yake.

 

“Mbona mipango yote ya usajili ilishakamilika muda mrefu na hizo kelele za Yanga tulikuwa tunasikia tu za kumteka Banda na kumsajli.

 

“Hivyo Banda tayari ameshasaini mkataba wa miaka miwili baada ya kufikia makubaliano mazuri na Simba leo (jana) jioni, alisema mtoa taarifa huyo.”Simba chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ juzi alisema: “

 

Usajili wetu tumepanga kuufanya kwa siri kubwa kutokana na ukubwa wa Simba ambao kama tulitangaza mchezaji tunayemtaka, basi klabu nyingine zitaingia katika vita.

 

Wakati huohuo, Championi Jumatano limepata taarifa za Simba kumuuza kiungo wake mshambuliaji Luis Miquissone klabu ya Al Ahly ya nchini Misri kwa dau la Dola 900, 000 (zaidi ya Sh Bil2) kwa miaka minne.

NA WILBERT MOLANDI NA CAREN OSCAR

Leave A Reply