The House of Favourite Newspapers

Bangala Aikamua Yanga Mamilioni Baada ya Kuongeza Mkataba Utakaomuweka Hadi 2024

0
                                    Kiraka wa Yanga, Mkongomani, Yannick Bangala

KIRAKA wa Yanga, Mkongomani, Yannick Bangala, baada ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, inaelezwa kwamba thamani ya mkataba huo ni shilingi milioni 400.

 

Bangala aliyefanikiwa kutwaa Tuzo ya Kiungo Bora wa Ligi Kuu Bara 2021/22, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utaendelea kumuweka Yanga hadi 2024 baada ya ule wa awali kutarajiwa kuisha 2023.

 

Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza beki wa kati na kiungo mkabaji, alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2021/22 akitokea FAR Rabat ya Morocco.

 

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa, kiraka huyo ameongeza mkataba huo baada ya yeye mwenyewe na meneja wake kufikia muafaka mzuri na viongozi wa timu hiyo.

 

Bosi huyo alisema kuwa, kiungo huyo baada ya kusaini mkataba huo, anakadiriwa kuchukua dau la zaidi ya shilingi milioni 400. Aliongeza kuwa, baada ya kumalizana na Bangala wapo katika mazungumzo na mshambuliaji wao, Fiston Mayele ambaye hivi karibuni ataongezewa mkataba.

 

“Hatutaki kumuachia mchezaji yeyote muhimu katika timu yetu kwa wale ambao mikataba yao wamebakiwa na miezi au mwaka mmoja.

 

“Hivyo tumemuongezea mkataba Bangala ambao rasmi utakuwa unamalizika mwaka 2024. Tunafurahia kuona akiendelea kubakia hapa,” alisema bosi huyo .

 

Akithibitisha hilo, Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said, alisema: “Hatutaruhusu mchezaji yeyote muhimu kuondoka Yanga. Kwa wale wote mikataba yao inatarajiwa kumalizika na iliyomalizika tutawaongezea.

Stori: Wilbert Molandi

Leave A Reply