Bao La Mayele Lampa Ugonjwa Kifaru

BAO alilofunga mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, limesababisha msemaji timu hiyo, Thobias Kifaru apate homa ya ghafla iliyomfanya akae kimya kwa muda kupambania afya yake.

 

Yanga na Mtibwa zilikutana hivi karibuni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa mkoani Morogoro ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Saido Ntibazonkiza na Fiston Mayele.

 

Ikumbukwe siku chache kabla ya mchezo huo, msemaji huyo aliweka wazi mikakati yao ya kuhakikisha wanaifunga Yanga ikiwemo kumzuia mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele kwa kumpa kazi kumkaba beki wao Ibrahim Ame lakini haikuweza kusaidia wasifungwe na mshambuliaji huyo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kifaru alisema kuwa amekuwa kimya kwa muda baada ya mchezo dhidi ya Yanga kwa kuwa alikuwa akiumwa baada ya kupata homa iliyotokana na maumivu ya kufungwa na Yanga.

 

“Tumeanza kukaa sawa kwa sababu tumefanikiwa kushinda mchezo wetu wa kwanza wa mzunguko wa pili dhidi ya Mbeya Kwanza lakini nilikuwa kimya kwa sababu niliumwa baada ya mchezo wetu na Yanga hivyo nikawa napambania afya yangu kwa kuamua kukaa kimya.

 

“Kiukweli sikupendezwa na matokeo yale hasa safu ya ulinzi ilikuwa hovyo kabisa, sikutaka kusema kama nilikuwa naumwa ila yale matokeo yalinipa maumivu makali sana kutokana na historia ya hii timu jinsi ambavyo tuliianzisha mwaka 1983 lakini inaoneka vijana hawajui maumivu tunayopata,” alisema Kifaru.

STORI: IBRAHIM MUSSA2174
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment