Bao moja tu, Tchetche aanza kuchonga

KIPRESTRAIKA wa Azam FC, Kipre Tchetche amefunga bao moja tu dhidi ya Prisons katika Ligi Kuu Bara, lakini ameanza majigambo kwa kusema bao hilo limefungua njia kutwaa tuzo ya mfungaji bora msimu huu.

Bao linalompa kiburi Tchetche raia wa Ivory Coast, alilifunga dhidi ya Prisons ambapo timu yake ilishinda mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam.

Katika mechi zilizochezwa hadi sasa na timu 16 za ligi kuu, wanaoongoza wana mabao mawili ambao ni Hamis Kiiza wa Simba, Donald Ngoma (Yanga), Atupele Green (Ndanda FC) na Miraji Athuman wa Toto Africans.

Tchetche alisema kuwa: “Nashukuru kwa kuanza vizuri msimu kwa kufunga bao kwenye mchezo wa kwanza na huu ni mwanzo mzuri kwangu kuelekea kuwa mfungaji bora.

“Furaha yangu ni kuona timu yangu inashinda kila mchezo, pia nitajituma kuhakikisha nafunga kila mara kwa manufaa ya timu na harakati zangu za kuwa mfungaji bora.”

JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778CHAMPIONI
Toa comment