The House of Favourite Newspapers

Barabara mpya lakini chafu!

0

Barabara ya Magufuli (1) Barabara ya Magufuli (2) Barabara ya Magufuli (3) Barabara ya Magufuli (4)

Pichani juu ni taswira za barabara ya Ali Hassan Mwinyi iliyopanuliwa ikiwa inatumika mbali na kujaa michanga.

BARABARA ya Ali Hassan Mwinyi kutoka Mwenge hadi Sayansi ambayo imepanuliwa kwa maagizo ya Rais Dk. John Pombe Magufuli imefunguliwa na inaanza kutumika na magari yote, lakini ni chafu, imejaa michanga ambayo inahatarisha uhai wa barabara hiyo!.

Mtandao wa Global umeongea na baadhi ya watumiaji ambao wamehoji iweje barabara hiyo iliyotengenezwa kwa mabilioni ya shilingi lakini mamlaka husika zishindwe kusafisha tu?

Rais Dk. Magufuli aliagiza kutumika kwa shilingi bilioni nne kupanua barabara hiyo kutoka Mwenge mataa hadi Morocco mataa na tayari kipande cha kati ya Mwenge na Kijitonyama kimeshakamilika.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY / GPL)

Leave A Reply