The House of Favourite Newspapers

BARACK OBAMA, HILLARY CLINTON WATUMIWA MABOMU

Image result for oBama and Hillary Clinton 

MARAIS wastaafu wawili wa Marekani, Bill Clinton, Barack Obama na Mbunge, Mazine Walters, ni miongoni mwa watu ambao wametumiwa mabomu ya siri kwenye vifurushi yaliyolenga kuwadhuru.

Kwa Waters, hii ni mara ya pili anatumiwa bomu la aina hiyo.

Hivi majuzi bomu liligunduliwa karibu na nyumbani kwa Bill na Hillary Clinton, na furushi jingine lililotiliwa mashaka lilitumwa kwenda nyumbani kwa Barack Obama, walisema polisi juzi.

Bomu jingine la aina hiyo lilitumwa kwa  George Soros,  tajiri na mtu maarufu kwa kutoa misaada ya kwa jamii ambaye pia ni mwanachama wa Democratic Party na mkosoaji mkubwa wa Rais Donald Trump.

Bomu lililotumwa nyumbani kwa Clinton lilikuwa limeandikwa jina la mkewe, Hillary.  Serikali inachunguza video za kunasa matukio kujua  furushi hilo lilifikishwa hapo kwa njia gani.  Familia za  Clinton na Soros zinaishi eneo la Westchester County.

Comments are closed.