The House of Favourite Newspapers

Barakah da Prince kuachia ngoma mfululizo

0

Baraka.jpgBaraka Da Prince

Said Ally, Dar es Salaam
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya Baraka Andrew ‘Barakah da Prince’ amesema anajipanga kutoa nyimbo mfululizo ili kujipa nafasi ya kujitangaza zaidi sambamba na kuwapa mashabiki wake burudani ya ukweli.
Barakah kwa sasa ‘ana-make headline’ katika ‘media’ mbalimbali za hapa nchini na mkwaju wake wa Siwezi alioutoa wiki chache zilizopita.
Akizungumza na Championi Jumatano, Barakah alisema ameamua kuchukua uamuzi huo ili kujitangaza zaidi kwa mashabiki wake sambamba na kuwapa ladha ya aina ya muziki anaofanya.
“Tayari nina mpango huo na nimeshajipanga kuhakikisha nawapa muziki mzuri mashabiki wangu kwa kutoa ngoma kadri nitakavyoweza na mpango huo unaweza ukawa baada ya kila miezi miwili,” alisema Barakah.

Leave A Reply