The House of Favourite Newspapers

Baraza la Mawaziri la Magufuli… wabunge matumbo joto

1

magufuliRais Dk John Pombe Magufuli.

Gabriel Ng’osha

WAKATI Rais John Pombe Magufuli akitegemewa kutangaza Baraza la Mawaziri wakati wowote kuanzia sasa, matumbo ya wabunge yamepata moto wakijiuliza kama watawezana na kasi yake endapo watateuliwa kuwemo.

Magufuli, ambaye Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimuita Tingatinga, ameweka wazi katika hotuba yake kwa Bunge kuwa hatamvumilia mtu mzembe na mvivu na kwamba watakaobainika kujihusisha na rushwa au ufisadi, watashughulikiwa.

Ingawa wabunge karibu wote walikuwa wakimshangilia kwa nguvu wakati wa hotuba yake hiyo, inadaiwa hamu ya kupata ulaji wa uwaziri inawafanya baadhi yao kuingiwa na woga, kwani ufanyaji kazi wa mazoea ndiyo unaowatesa.

“Nakuambia hapa wabunge, hasa wale wenye ndoto za kuteuliwa uwaziri wana wasiwasi kama wataweza kweli kwenda na kasi ya huyu jamaa, maana anaonekana kuwa siriaz sana na kazi. Hili liko wazi maana wengi walizoea kuona nafasi za juu kiuongozi wanazitumia kwa masilahi yao,” kilisema chanzo chetu katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Inadaiwa wengi wa wanaotegemea kupata uwaziri wana hofu kwa sababu wanaamini mzigo watakaopewa utakuwa mkubwa kuliko tabia na hulka zao.

Rais Magufuli ameahidi kuteua Baraza dogo la Mawaziri litakalokuwa limesheheni wachapakazi na katika kukabiliana na vitendo vya rushwa na ufisadi, alisema kazi hiyo ataifanya kwa dhati.

Hata hivyo, mbali na jina la Tingatinga hivi sasa mtaani amepewa jina jipya la Mtumbua majipu licha ya kuwa kitendo hicho huleta maumivu.

1 Comment
  1. Edward kiboko says

    Dk magufuli uko vizuri sana na mungu akupe afya njema ktk utendaji wako wa kazi pamoja na uongozi wako wote amina

Leave A Reply