Baraza Yatoa rai Kwa Wadau wa Sanaa na Wasanii Kuheshimu Misingi ya Kiungwana
Baraza la Sanaa la Taifa linalaani tukio lililovuriga utumbuizaji wa Mwanamuziki Zuhura Othman (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na mashabiki wasiokuwa waaminifu katika tamasha la Wasafi Festival Septemba 28, 2024 lililofanyika katika mkoa wa Mbeya.
Aidha, Baraza linatoa rai kwa wadau wa sanaa na wasanii kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyo na tija, pamoja na hayo, waandaaji wa matukio wanatakiwa kuzingatia uwepo wa mazingira salama kwa wasanii na wadau wake wakiwa katika majukumu yao.