Barbara: Msimu Mpya Mambo mapya

BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba, ameweka wazi kuwa wanakwenda kuanza msimu mpya wa 2021/22 kwa mambo mapya jambo ambalo litakuwa ni rekodi kwa timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Barbara alisema kuwa wanatambua juu ya umuhimu wa mechi zao za ligi pamoja na mipango iliyopo, hivyo watakuwa tofauti katika kila jambo.

 

“Nadhani ni msimu mpya, hapo sisi tunapaswa kuwa na mambo mapya, kwetu kila kitu ni kipya, kuanzia mbinu, wachezaji wetu nao wana mipango mipya.

 

“Jambo la msingi kwa sasa ni mashabiki kuendelea kuwa nasi bega kwa bega kwani Simba ni timu kubwa, hivyo inahitaji kuwa na matokeo makubwa pia katika yale ambayo yanafanyika,” alisema Barbara.

 


Toa comment