The House of Favourite Newspapers

Barca yaandaa silaha tatu kunyanyasa UEFA

BARCELONA inajidai na silaha tatu ambazo inaamini zitakazowasaidia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2018/19.

 

Wakifanikiwa kufanya vizuri katika mechi za mashindano haya watatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya fainali itakayochezwa katika uwanja wa Wanda Metropolitano, Juni 1, mwaka huu. Mara ya mwisho kwa Barcelona kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa ilikuwa kwenye msimu wa 2014/15.

 

Mtihani wa kwanza kwenye michuano hiyo wanaokabiliwa nao ni kuvuka dhidi ya Manchester United kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mechi ya kwanza baina ya timu hizo mbili itachezwa Aprili 10 kwenye Uwanja wa Old Trafford wakati ile ya marudiano itafanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Nou Camp. Barcelona sasa wanamini silaha tatu zitawasaidia kutwaa taji hilo msimu huu.

 

Silaha ya kwanza ni uwepo wa mfungaji hatari, Lionel Messi, ambaye yupo moto kwani ametupia mabao nane katika mashindano hayo na ndiyo anaongoza. Pamoja na kupiga mabao, Messi pia yupo vizuri likija suala zima la kutoa asisti.

 

Silaha yao nyingine ni rekodi ya kutofungwa katika Uwanja wao nyumbani wa Nou Camp. Barcelona ina rekodi ya kutofungwa katika mechi 30 za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika uwanja huo. Silaha yao nyingine ni kipa Ter Stegen, ambaye anatajwa kama miongoni mwa makipa bora duniani.

 

Stegen ametokea kuokoa hatari ambazo zimeisaidia kwa kiasi kikubwa kwa Barcelona kuibuka na ushindi kwenye mechi ngumu.

SIMBA Wafunguka Kumuuza KAGERE “Anapendwa Hadi na Watoto”

Comments are closed.