The House of Favourite Newspapers

Barnaba Ataja Kinachomuingizia Mkwanja Mrefu

STAA wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kipekee, Elias Barnaba amesema kuwa kitendo cha kuwatungia mastaa ngoma zao hasa wa kike kimemfanya kutengeneza mkwanja mrefu.

Akichonga na Risasi Vibes, Barnaba ambaye kwa sasa amejitoa THT na kuanzisha lebo yake ya Hightable Sound alisema, hawezi kutaja mpaka sasa amepata kiasi gani lakini wasanii wa kike wengi aliowatungia ngoma wamekuwa wakimlipa vizuri.

“Ukiachilia mbali mkwanja ninaoupata kupitia studio na lebo yangu ya Hightable, kazi zangu za muziki, kingine kikubwa ni hawa wasanii ninaowatungia nyimbo, wamekuwa wakinipa mkwanja mrefu,” alisema Barnaba ambaye amewahi kuwatungia nyimbo mastaa kibao wa kike akiwemo Linah, Shilole, Lulu Diva, Recho na wengineo.

Comments are closed.